Mwenyekiti wa vijana wa CCM(UVCCM) mkoa wa Rukwa ndugu
Ramadhani Shabani leo hii akizungumza kwenye mkutano uliokuwa umeandaliwa na
idara ya vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Rukwa amesisitiza zaidi katika kuwasihi
vijana wa CCM kutokukaa kimya pale viongozi wakuu pamoja na viongozi wa chama
hicho wengine wanapovunjiwa heshima,Amesema atakayemvunjia heshima mhe Rais Dkt
John Pombe Joseph Magufuli,Mwenyekiti wa CCM taifa pamoja na katibu mkuu wa CCM
taifa ndg Dkt Bashiru Ally Kakurwa nae heshima yake ivunjwe haraka iwezekanavyo
kwani ulinzi wa heshima ya mwenyekiti wetu wa chama taifa pamoja na katibu mkuu
wa CCM taifa haipaswi kuwa mjadala bali daima inatakiwa kulindwa kwa gharama
yoyote ile.
Aidha amesema kuwa Inawapasa wapinzani watambue na kuelewa
wazi kabisa kwamba hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuwakataza wao wasiikosoe
serikali na mhe Rais ila je?ni kwa mfumo upi wanaoutumia kuikosoa serikali ya
CCM na viongozi wake haiwezekani na hakika kama vijana wa CCM mkoa wa Rukwa
hatutakaa kimya na kuvumilia matusi,kejeri,vitimbi na upotoshwaji mambo wa
makusudi kabisa unaofanywa na wapinzani kwa kisingizio cha mwamvuli wa haki ya
kukosoa and freedom to speech.
Natoa rai kwa kiongozi mwenzetu na kijana mwenzetu anayejiita
mwenyekiti wa Bavicha taifa ndugu *Patrick Ole Sosopi* kuacha kushughulika na
mambo ya ovyo kuacha kucheza ngoma ya kina Freeman Mbowe kwani mambo hayo
hayana maslahi kwa vijana kama uasisi wa Bavicha ulivyomaanisha, tumia muda
wako kuona ni namna gani unaweza kuungana na UVCCM ambayo ipo chini ya kiongozi
makini kabisa.
Comrade Kheri Denice James UVCCM yenye agenda moja tu!ya
kushughulika na kero za vijana wa taifa hili, UVCCM inayoshughulika na
kuhakikisha halmashauri zinatoa mikopo kwa vijana, UVCCM inayohakikisha vijana
waliojiajiri katika biashara ndogo ndogo hawasumbuliwi,UVCCM inayoshughulika na
kuhakikisha vijana wasomi wanaotakiwa kwenda vyuoni na kustahili kupata mikopo
wanapata mikopo hiyo kwa ujumla UVCCM yenye agenda na vijana na sio Bavicha
yenye kuwapeleka vijana kwenda kufanya maigizo pale mahakamani.
Imetolewa Na;-
Idara Ya Hamasa Na Chipukizi Mkoa Wa Rukwa.
0 comments:
Post a Comment