Haki ya
kukosoa na na kujieleza inalindwa na katiba ya JMT 1977 na sio miongozo ya
UVCCM .
Haki ambayo
UVCCM Rukwa wameitumia kumkosoa mwenyekiti BAVICHA Taifa Patrick Olesosopi*
ndio haki hiyo hiyo ambayo *Pattrick Olesosopi ameitumia kumkosoa rais Magufuli
na kwamba haki zote zinalindwa na katiba ya JMT.
BAVICHA mkoa
wa Rukwa tumeshitushwa na kushangazwa na uelewa mdogo wa UVCCM mkoa wa Rukwa
juu ta tamko lao walilo litoa Jana ya 8 Desemba 2018 katika mahafali ya vyuo
vikuu CCM. Katika tamko lao, pamoja na mambo mengine *wametoa vitisho* vikali
kwa wale walio waita wakosoaji wa Rais Magufuli na Dr.Bashiru na msingi wa hoja
zao dhaifu ilikua ni kujibu tamko LA Mwenyekiti BAVICHA Taifa.
BAVICHA Rukwa
tuanawashauli UVCCM kwamba,ikiwa wanaamini ukosoaji wa Magufuli na Bashiru ni
kinyume cha katiba na sheria ya Nchi waende mahakamani kuliko kutoa vitisho
kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai.
UVCCM
wanapaswa kujibu hoja za msingi zilizotolewa na Sosopi kuliko kujikita katika
vitisho.
Na UVCCM
Rukwa haipaswi kujikita kulinda walichokiita heshima ya Magufuli na Bashiru,
*wanapaswa kuwa na wivu wa kulinda heshima ya Nchi badala ya kile walichokiita
heshima ya Magufuli na Bashiru*
Kwetu sisi
BAVICHA Rukwa ,heshima tuatalinda heshima ya Nchi yetu kwa gharama yoyote dhidi
ya wale wanaopenda uonevu,na kuamini katika utawala wao kuliko utawala wenye
misingi ya mifumo ya kisheria tuliyonayo kwasasa.
BAVICHA Rukwa
pia tunapenda kutoa pole kwa Mwenyenyikiti wetu wa chama Taifa Mh Freeman Mbowe
Mbunge pamoja na Mh Ester Matiko Mbunge ambao wako Mahabusu kwa sababu tu ya
kupigania Haki,Uhuru,Usawa na Demokrasia ya kweli katika taifa letu.Tunaamini
hakuna vitisho vitakavyotufanya turudi nyuma katika mapambano haya .
Hakuna vita
nyepesi ila hili nalo litapita na mapambano haya tutayashinda .
BAVICHA Mkoa
wa Rukwa tunaunga mkono na kulitekeleza agizo la mwenyekiti wetu BAVICHA taifa,
UVCCM tunafahamu bado ni wachanga sana tunawataka waendelee kujifunza uongozi
kwa kumuelewa mwenyekiti Ole Sosopi ambaye ni kiongozi si wa kiwango chenu.
Imetolewa na;
Aida Joseph Khenan*
Mwenyekiti BAVICHA Mkoa Wa Rukwa.
Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255
755747892 Kapolanewz tv.
0 comments:
Post a Comment