Tamasha la Wasafi Festival lililokuwa likifanyika jana (Jumamosi) usiku limeahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha na hivyo kushindwa kuendelea.
Hata hivyo onesho hilo lililokuwa likifanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini hapa liliahirishwa huku wasanii Country Boy, Queen Darlin, Gigy Money, Lavalava na Young Killer wakiwa tayari wameshamaliza kupiga shoo zao jukwaani.
Kutokana kuahirishwa kwa tamasha hilo Msanii Diamond Platnumz alipanda jukwaani na kuwaomba radhi mashabiki waliokuwa uwanjani hapo na ambapo alitangaza kuwa Tamasha hilo litaendelea tena uwanjani hapo leo Jumapili jioni kuanzia saa 10:00.
0 comments:
Post a Comment