News Alert ! JE ULIPITWA NA HII WATU 12 WAFARIKI BAADA YA HIACE KUTUMBUKIA ZIWA VICTORIA



Watu 12 wamefariki dunia na watatu wameokolewa wakiwa salama baada ya Toyota Hiace kutumbukia Ziwa Victoria katika kivuko cha Kigongo Feri wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema katika ajali hiyo watu watatu wameokolewa wakiwa hai.

Msangi amesema walionusurika wameokolewa na wananchi ambao ni wataalamu wa kuogelea.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) inayosimamia kivuko hicho,, Ferdinand Mshama amesema gari hilo linafanya safari kati ya Buhongwa jijini Mwanza na kivukoni hapo.

Amesema ajali hiyo imetokea kutokana na gari hilo kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki hivyo liligonga geti la kivuko na kutumbukia ziwani.

“Ni kweli gari limetumbukia, lilikuwa likitokea Buhongwa kupeleka abiria kivukoni, kabla dereva hajapaki lilifeli breki,” amesema na kwamba dereva alipita upande wa magari makubwa.

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment