WANANCHI wa
kijiji cha Kasinde kilichopo wilaya
ya Momba Mkoani
Songwe wameingia kwenye
wakati mgumu baada ya
kuwauzia wafugaji maeneo
ya hifadhi ya
wilaya ya Kalambo
mkoani Rukwa kinyemela
na kupelekea kuibuka
kwa mgogoro baina
yao na wafugaji.
Wananchi
wa kijiji cha
kasinde Kilichopo wilaya
ya Momba wanapakana na hifadhi
ya kijiji cha
mlenje kata ya
legezamwendo wilaya ya
kalambo, ambapo kutokana na hifadhi
hiyo kuwa mpakani wananchi
hao wamejikuta mikoni
mwa jeshi la polisi
baada ya kuuza maeneo ya hifadhi hiyo bila
kuhusisha serikali .
Hali hiyo
imefanya mkuu wa
wilaya ya kalambo
mkoani hapa Julith Binyura kuingilia kati swala
hilo kisha kufika
kijijini hapo na kuitisha mkutano
wa hadhara na kutoa
siku saba kwa wafugaji
walivamia hifadhi hiyo
kuondoka maramoja.
Awali akiongea
mbele ya mkutano
huo diwani wa kata
ya legeza mwendo Mwakyusa
Sijera lameki, amesema maeneo
hayo yalikuwa yakiuzwa
kuanzia shilingi milioni
moja (1,000,000/=) hadi milini mbili (2,000,000/=)na kuwa Zaidi
yaa familia 20 za wafugaji ziliuziwa
maeneo hayo kinyemela.
0 comments:
Post a Comment