ZAIDI ya nyumba 10 zimeezuliwa katika kijiji cha Matai asilia kata ya Matai wilaya ya kalambo mkoani Rukwa baada ya mvua kubwa ya mawe iliokuwa imeambatana na upepo mkali kunyesha na kupelekea watu kuumia na wengine kukosa mahali pa kuishi.
Wakiongea na kituo wahanga wa tukio hilo wamesema mpaka sasa wahawana mahali pa kuishi kutokana na makazi yao kuharibiwa vibaya na kuiomba serikali kuwapatia makazi ya muda wakati wanaendelea na jitihada za ukarabati wa makazi yao.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Isack sawala amesema baada ya kupata taarifa hiyo walipeleka taarifa wilayani na kuwa watu wengine wamekimbizwa kwenye kituo cha afya cha matai kwa ajili ya matibabu Zaidi.
Katibu tawala wilayani humo Frank Sichalwe , ambae licha ya kukili wazi kutokea tukio hilo amesema nyumba 11 zimeezuliwa na kati hizo nane 8 zimeboka kabisa nakuwa majeruhi wanaendelea vizuri .
Aidha sichalwe ametumia fulsa hiyo kuwataka wananchi kujenga nyumba imara kwa lengo la kusaidia kuondokana na kujirudia kwa matukio hilo.
Hata hivyo hilo ni tukio la tatu kutokea kwenye tarafa hiyo ambapo tukio la kwanza lilitokea maeneo ya kasisiwe, kateka na hatimaye kutokea kijijini.,
0 comments:
Post a Comment