Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameishauri
benki ya NMB kufungua tawi katika bonde la Ziwa Rukwa ili kusogeza huduma hiyo
karibu na wananchi ambao shughuli zao kubwa za kiuchumi ni kilimo cha mahindi, mpunga
pamoja na uvuvi.
Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutaepusha matukio ya uvamizi
na mauaji yanayofanywa na baadhi ya watu wanaowavizia wakulima na
wafanyabiashara wanaoweka fedha majumbani mara tu baada ya mauzo ya mazao yao.
“Mimi nashauri Benki ya NMB muwe na Tawi huku, si lazima
kuwa na jengo, hata ile Mobile Banking ambayo mwananchi anaweza kupata huduma
zote za kuweka na kutoa fedha katika gari hiyo, ili fedha zao hawa ziwe katika
mikono salama,” Mh. Zelote Alisema.
Ametoa ushauri huo katika ufunguzi wa siku ya huduma kwa
wateja iliyofanywa na benki ya NMB kanda ya nyanda za juu katika Kijiji cha
Mfinga, kata ya Mfinga, Wilaya ya Sumbawanga, kabla ya kukabidhi vifaa vya
shule pamoja na hospitali vyenye thamani ya Shilingi milioni 20.
Sambamba na hilo Mh.Zelote amewahamasisha wakulima pamoja na
wafanyabiashara wa Kata ya Mfinga kufungua akaunti benki na pia kujiunga katika
vikundi ili kuwa na urahisi wa kupata mikopo
na kuweza kuwainua kiuchumi.
“Mbali na kuhifadhi fedha pia benki inatoa mikopo kwaajili
ya kujiendeleza na hatimae kuwainua wakulima waweze kuongeza thamani ya mazao
yao na kupata soko pana hasa katika awamu hii inayoongozwa na Rais Dk. John
Pombe Magufuli inayohamasisha uchumi wa viwanda kwa taifa,” Alisema.
Aidha aliwataka viongozi wa Kijiji na wanufaika wa vifaa
hivyo kuvitumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa, ikiwemo kuwahudumia
wananchi bila ya bugudha na kuonya kuwa wananchi wasiogope kuwashitaki
watumishi wanaowahudumia kwa viburi.
Awali akisoma taarifa fupi ya Benki ya NMB Mkurugenzi wa
Huduma kwa wateja makao makuu ya benki hiyo Richard Makungwa alisema kuwa Benki
ya NMB hutenga asilimia moja ya mapato kwa mwaka ili kuirudishia jamii na
kuweza kuisaidia katika mambo mbalimbali ikiwemo elimu na afya.
“Kwa kuunga mkono juhudi za Rais wetu tumeamua kama Benki
kutoa kompyuta 7, vitanda 8 vya kulalia, vitanda 4 vya kujifungulia, magodoro 8
pamoja na mabati 204 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 20
vilivyotolewa na benki hiyo kama marejesho ya faida kwa wateja watu,” Alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho Godfrey
Kalungwizi aliahidi kuvisimamia vifaa hivyo na kuendelea kuwahamasisha wananchi
kuchangia katika shughuli za kimaendeleo.
NMB2 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda
Suti ya Ugoro) akikabidhi Kompyuta kwa Afisa Elimu Manispa ya Sumbawanga
Silvestor Mwenekitete katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja katika Kijiji
cha Mfinga, Wilayani Sumbawanga.
NMB3 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda
Suti ya Ugoro) akikabidhi vitanda kwa mganga mfawidhi zahanati ya Mfinga
Ephraim Matekele (shati ya draft) katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja
katika Kijiji cha Mfinga, Wilayani Sumbawanga.
NMB4 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda
Suti ya Ugoro) akikabidhi vitanda kwa mganga mfawidhi zahanati ya Mfinga
Ephraim Matekele (shati ya draft) katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja
katika Kijiji cha Mfinga, Wilayani Sumbawanga.
NMB5 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda
Suti ya Ugoro) akiendeleza ujenzi kwa kuweka tofali katika jengo la shule ya
msingi Mfinga waliopewa mabati 204 na Benki ya NMB.
NMB6 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda
Suti ya Ugoro) katika picha ya pamoja na viongozi wa NMB pamoja na Wanafunzi wa
Shule ya Msingi Mfinga, Wilayani Sumbawanga.
0 comments:
Post a Comment