BREAKING: Basi lenye Wanafunzi zaidi ya 20 lapinduka Arusha ( picha5 )

 

Asubuhi ya May 6, 2017 imeripotiwa ajali iliyotokea Mlima Rhotia, Karatu mkoani Arusha ikuhusisha basi la Wanafunzi ambao walikuwa wanakwenda kufanya mtihani wa ujirani mwema.
Taarifa za awali zinasema kuwa Dereva wa basi la wanafunzi wa Shule ya LuckVicent alishindwa kuliongoza vizuri basi hilo wakati akikata kona kwenye mteremko hivyo likaingia kwenye korongo.
 

Kamanda wa Polisi Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea ajali hiyo akisema taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo zitatolewa baadae lakini taarifa zinasema Watoto 31 na Walimu wamefariki dunia.




Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment