BREAKING: Benki kuu Tanzania yafuta leseni ya Benki ya FBME By Peter kapola on May 8, 2017

 

Taarifa ambayo imetolewa na Benki kuu ya Tanzania leo May 8 2017 imesema mnamo tarehe 24 July 2014 Benki Kuu ya Tanzania iliiweka chini ya usimamizi maalumu (statutory management) FBME Bank Limited (FBME). 

Uamuzi huo wa Benki Kuu ulitokana na notisi iliyotolewa July 15 2014 na Taasisi ya Marekani inayopambana na uhalifu wa kifedha “the US Financial Crimes Enforcement Network” kwa kifupi FinCEN, iliyoituhumu FBME kuwa ni taasisi inayojihusisha na biashara ya utakatishaji wa fedha haramu (money laundering) na hatua ya Benki Kuu ya Cyprus kuliweka tawi la FBME lililopo nchini Cyprus chini ya uangalizi maalumu (special administration). 

Katika Notisi hiyo FinCEN ilitoa kusudio la kuifungia FBME kutotumia mfumo wa kibenki wa Marekani (US financial system) ambapo tarehe 29 Julai, 2015, FinCEN ilitoa uamuzi wa kuifungia FBME kutumia mfumo wa kibenki wa Marekani. 

FBME walifungua kesi huko Marekani (US District Court for the District of Columbia) wakiiomba Mahakama kutengua uamuzi wa FinCEN ambapo hatimaye April 14 2017 Mahakama ilitoa uamuzi ambao unairuhusu FinCEN kuendelea na utekelezaji wa uamuzi wake wa mwisho (Final Rule) ambao unaifungia benki ya FBME kutumia mfumo wa kibenki wa Marekani.

Uamuzi huo wa Mahakama unaongeza athari kwa kiwango kikubwa katika uendeshaji wa FBME kwa kuwa haitaweza tena kufanya miamala ya kibenki ya kimataifa na kupata huduma za mifumo ya kibenki na hivyo itashindwa kutoa huduma muhimu kwa wateja wake kwa mujibu wa leseni waliyopewa.

Kwa kuzingatia athari zinazotokana na uamuzi wa mwisho wa FinCEN, kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 58(2)a, 11(3)(i), 61(1) na 41(a) vya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imesimamisha shughuli zote za FBME Bank Limited kufuta leseni yake ya kufanya shughuli za kibenki, kuiweka chini ya ufilisi na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kama mfilisi kuanzia tarehe 8 Mwezi Mei, 2017

Kufuatia Benki Kuu kufuta leseni hiyo kuwa Mfilisi kuanzia tarehe 8 Mei, 2017, taarifa inatolewa kwa wenye amana, wadai na wadaiwa kuwa wawe wavumilivu wakati Mfilisi akiandaa utaratibu wa kushughulikia stahiki zao. 

Mfilisi kwa wakati muafaka atawafahamisha wenye amana, wadai na wadaiwa utaratibu wa malipo wa madai, ulipaji wa madeni na taratibu nyingine zitazohitajika kwa mujibu wa sheria na kwa maelezo ya ziada kuna mawasiliano ya Mkurugenzi, Bodi ya Bima ya Amana kwa anuani ifuatayo:
2 Mtaa wa Mirambo
 
Benki Kuu Makao Makuu, Ghorofa ya Saba, Mnara wa Kaskazini 11884, Dar Es Salaam
Simu: +255(0)22 2235390
Nukshi: +255(0)22 2234200
Barua Pepe: info@bot.go.tz

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment