Taarifa kutokea Jeshi la Polisi Dodoma
May 6, 2017 ni kuhusu matukio mawili tofauti yaliyofanyika mkoani hapo
yakihusisha kukamwatwa kwa watuhumiwa watano huku wanne kati yao
wakihusika na matukio ya ujambazi.
Kamanda wa Polisi Dodoma Lazaro Mambosasa amesema…>>>’Katika
tukio la kwanza Polisi inamshikilia Jumaa Ndosa mkulima wa Gairo,
Morogoro aliyekamatwa akiwa na gunia moja la mirungi lenye uzito wa kilo
50 alizokuwa akisafirisha kwa kutumia pikipiki‘
‘Tukio la pili Polisi
katika uchunguzi uliofanywa na Polisi katika kijiji cha Kibakwe Wilaya
ya Mpwapwa katika nyumba ya Msafiri Philipo na Frank Mapembe
tulifanikiwa silaha tatu aina ya Gobore na risasi aina ya chuma 70
zilizokuwa zikitumika kinyume cha sheria‘- Lazaro Mambosasa
0 comments:
Post a Comment