Wauguzi na
madaktari mkoani Rukwa wametakiwa kufanya kazi ya utabibu kwa kufuata misingi
na maadili ya fani yao.
Hayo
yamesemwa leo na mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Rukwa ZELOTHE STEVENI katika maadhimisho
ya siku ya wauguzi duniani ambayo kimkoa yamefanyika mjini sumbawanga katika
Hospitali ya DR,Atman klistu mfalume.
Zelothe amesema
maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani iwe ngao ya kuwakumbusha wauguzi
majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kulinda afya za wananchi.
Kwa upande
wao, wakazi wa sumbawanga wameelezea
kufurahishwa na maadhimisho hayo kufanyika katika wilaya hiyo, huku wakitoa
malalamiko juu ya unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya wauguzi katika vituo vya
afya.
Tazama video hapa chini wauguzi mkoani Rukwa wakicheza kwaito kwa pamoja..........
0 comments:
Post a Comment