MAHAKAMA
ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imehukumu mkazi wa kijiji cha Kamsisi,
Richard Chambanenge (20) kutumikia kifungo cha maisha baada ya kukiri
kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita akiwa ni binti
wa tajiri yake.
Mshitakiwa huyo alikuwa akifanya kazi ya
kibarua katika shamba la tumbaku mali ya Joseph Felix ambaye ni baba
mzazi wa mtoto huyo wa kike. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa
Mahakama ya Wilaya ya Mlele, Teotimus Swai alishangazwa na uamuzi wa
kuvunja shitaka kwa kukiri kosa hata baada ya mashahidi wanane walioitwa
na upande wa mashtaka mahakamani hapo.
“Pamoja na mshtakiwa kukiri kosa… kwanza namshangaa kwa kuwa alikana
kosa alipofikishwa mahakamani hapa kwa mara ya kwanza na upande wa
mashitaka waliita mashahidi wanane kutoka ushahidi wao mahakamani hapa,
na leo hii mshtakiwa amevunja shtaka kwa kukiri kosa lake,” alisema
Swai.
Akaongeza, “Pamoja na uamuzi wake huo, hakuna mbadala wa adhabu isipokuwa utatumikia kifungo cha maisha jela.”
Awali Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Bakari Hongoli alidai
mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo, Januari 20, mwaka
jana saa tisa mchana ambapo alivizia na kumbaka msichana huyo wakati
wakilinda ngedere katika shamba la tumbaku ambalo ni mali ya baba yake
mzazi.
0 comments:
Post a Comment