Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Job Ndugai
amewakumbusha wabunge wa vyama vya upinzani hasa vinavyounda UKAWA
umuhimu wa jamii kukaa pamoja, kujadiliana na kumaliza tofauti zao.
Ndugai ambaye ni mmoja wa wabunge wa Bunge la 11 aliyasema hayo baada ya
baadhi ya wabunge hasa wa upinzani kususia futari aliyoiandaa siku ya
Jumanne kwa ajili ya wabunge wote. Kiongozi huyo wa juu wa mhimili huo
alisema kuwa licha ya jukumu zito la kujadili na kupitish bajeti ya
serikali ya 2017/2018, ushirikiano kwa jamii ni muhimu.
Jambo hilo lilmfanya asiwe na raha na kuamua kuzungumzia ndani ya bunge
kwa upole kabisa ambapo alisema kuwa, baada ya kuhudhuria futari
iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Jumatatu, na baada ya kuwepo tetesi za
kususia ya kwake alisema, amejifunza kuwa baadhi wamekatazana kuhudhuria
shughuli kama hizo.
“Lakini nikajifunza kitu kimoja ambacho sikupenda kukisema, ila nikiseme
hapa kidogo. Kuna wenzetu wamekatazana rasmi kuhudhuria shughuli kama
hizi.”
Ndugai aliyasema hayo Jumanne wakati akihitimisha kipindi cha maswali na
majibu kabla ya kupisha mapumziko na kisha kupigiwa kura kwa bajeti ya
serikali.
"Bunge linaendeshwa kwa mawasiliano ya namna mbalimbali baina ya wabunge
na uongozi. Endapo kuna jambo linakwaza na kusababisha watu wasipate
futari pamoja, ni vizuri wakae pamoja na kuondoa jambo hilo,"
alizungumza Ndugai.
Licha ya kutoa tahadhari hiyo, Ndugai alisema kuwa wabunge hao wana
uhuru wa kufanya hivyo (kutohudhuria) kama wanaona ni sawasawa.
“Siyo mwezi wa chuki na kubaguana. Niwakaribishe tena kwenye futari kwa
watakaoweza kufika. Watakaoshindwa In Sha Allah, kila la heri.
Tutaendelea kuwa pamoja mjengo huu huu,” alisema Spika Ndugai
akihitimisha nasaha zake.
0 comments:
Post a Comment