MLINZI WA SHULE YA SEKONDARI JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA


 

Mahakama ya Wilaya ya Mlele imemuhukumu mlinzi wa Sekondari Ilela, George Sikoki kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa umri wa miaka 16.
Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Hakimu Mkazi Mfawidhi Teotimus Swai baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa.
Mwendesha mashtaka, Baraka Hongoli alidai katika ushahidi mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 27 saa 7:30 usiku.
Alidai Sikoki ambaye ni mlinzi wa shule hiyo iliyopo tarafa ya Inyonga wilayani hapa alitenda kosa hilo wakati ambao wazazi wa mtoto huyo wakiwa safarini naye alikuwa akilala peke yake.
Upande wa mashtaka ulidai mshtakiwa alikwenda nyumbani kwa mtoto huyo na kuvunja mlango kisha kumtishia kumuua iwapo angepiga kelele hivyo kumbaka na kutokomea kusikojulikana.
Ilielezwa mahakamani kuwa binti huyo akiwa na maumivu makali, huku akitokwa damu sehemu za siri alijikongoja hadi kwa jirani na kutoa taarifa ndipo alipopelekwa hospitali kwa matibabu.
Hongoli alidai baada ya mshtakiwa kukamatwa alikiri kosa hilo kwa maandishi wakati akihojiwa kituo cha polisi, lakini alipofikishwa mahakamani alikana.
Upande wa mashtaka ulipeleka mahakamani mashahidi sita akiwamo daktari kuthibitisha shtaka hilo ambapo waliithibitishia mahakamani bila kuacha shaka
 

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment