picha na peter kapola
UGONJWA
wa kipindupindu umelipuka katika kijiji na kata ya Samazi
katika Mwambao wa ziwa Tanganyika wilaya ya Kalambo mkoani
Rukwa na kusababisha kifo cha mtoto mmoja lina protas miaka 5
na wengine 16 wamelazwa kwenye zahanati ya kijiji hicho.
Akiongea
na kituo hiki ofisni kwake afisa tarafa ya Kasanga wilayani
humo Peter Mankambila , amesema chanzo cha ugonjwa huo
kimetokana na wavuvi waliokuwa wametokea katika kijiji cha
Mpasa kilichopo wilaya jilani ya Nkas,ambao walifika kijijini
hapo kwa shughuri za uvuvi na kuwambukiza wengine.
Amesema
ugonjwa huo uligundulika june 16 ,2017 na kuwa mpaka sasa
watu wapatao 16 wamelazwa kwenye zahanati ya kijiji hicho kwa
matibabu zaidi .
Afisa
afya wilaya humo , Andondile Mwakilima ambae licha ya
kukili wazi kuwepo adha hiyo amesema, mpaka sasa watu (8)
wameruhusiwa kurudi nyumbani na watu 8 wanaendelea kupatiwa
matibabu zaidi na kuwa mpaka sasa wanaendelea kuhamasha jamii
kuchimba vyoo vya kudumu kwa lengo la kujiepusha na ugonjwa
huo.
Mkuu
wa wilaya hiyo , Julith Binyura , ambae licha ya kukili wazi
kuwepo adha hiyo amewataka wanchi wanao ishi kwenye mwambao wa
ziwa hilo kutumia maji safi na salama kwa lengo la kujiepusha
na ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment