KATAVI
Jeshi la Polisi Mkoani katavi
katika kuhakikisha linadumisha amani na
usalama msimu huu wa Sikukuu limesema litatumia vikosi vyake vyote kusimamia
amani na usalama maeneo mbalimbali zikiwemo kumbi na sehemu zenye mkusanyiko wa
watu wengi.
Kauli hiyo imetolewa leo na kaim kamanda wa polisi mkoani Katavi Benedicto Mapujila wakati akizungumza na Chemchemi redio fm kutaka kujua namna gani jeshi Hilo lilivyojipanga katika kuimarisha ulinzi hasa kwa siku hiyo ya siku kuu.
Hata hivyo kamanda Mapujila
ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kusherehekea siku kuu hiyo kwa amani
bila kufanya vurug.
0 comments:
Post a Comment