WAKAZI wa kijiji cha Mkole kata ya Nkomolo wilayani Nkasi
mkoani Rukwa wamepata taharuki baada ya Tembo wapatao 9 kuvamia katika kijiji
hicho wakitokea katika poli la hakiba la Lwafi.
Diwani wa kata
hiyo Egyd Ngomeni amesema tembo hao waliingia kijijini hapo majira ya saa 2 asubuhi ambapo wananchi
wake walichukua hatua
ya kujifungia
ndani na familia
zao kwa kuogopa
madhara ya wanayama
hao na kusema
tembo hao wamekuwa
wakijitokeza kila mwaka
katika maeneo hayo .
amesema kufuatia hali
hiyo alitoa taarifa
kwenye uongozi wa halmashauri ya wilaya na Poli la hakiba la
Lwafi na baada ya muda askari wanyama pori wa halmashauri na wale wa hifadhi ya
pori la hakiba la Lwafi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuwafukuza kwa
kupiga lisasi angani.
Mkuu wa wilaya hiyo
saidi mtanda , amethibitisha kuwepo
adha hiyo na
kusema tembo hao walifika
kijijini hapo kwa
lengo la kutafuta
maji na si
vinginevyo .
0 comments:
Post a Comment