Rais
Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo amempongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuonesha mfano
bora katika Bara la Afrika katika kusimamia uchumi na kutetea maslai ya
nchi katika uwekezaji.
Mhe.
Rais Mstaafu Obasanjo ametoa pongezi hizo leo tarehe 20 Juni, 2017 muda
mfupi baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Rais Mstaafu Obasanjo amesifu juhudi za Mhe. Rais Magufuli
kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali
duniani na kusimamia ipasavyo sera ya kuhakikisha nchi inanufaika,
badala ya kuacha wawekezaji wakijinufaisha wenyewe na nchi kuambulia
kiasi kidogo cha mapato.
“Nimepita
katika nchi kadhaa zikiwemo Msumbiji, Malawi na sasa nipo hapa
Tanzania, na huko kote nazungumzia masuala ya uchumi na namna nchi zetu
za Afrika zinapaswa kunufaika na uwekezaji katika maeneo mbalimbali.
“Uchumi
wa Tanzania unakwenda vizuri sana, na juhudi za Mhe. Rais Magufuli za
kuhakikisha nchi yake inanufaika na uwekezaji ni suala muhimu sana na la
mfano, ameonesha mfano mzuri kwa viongozi wa Afrika na hii ndio njia
pekee itakayotuwezesha kukuza uchumi wetu, hatuwezi kuendelea kuwaacha
wawekezaji wananufaika wao na sisi kuambulia kiasi kidogo sana” amesema Mhe. Rais Mstaafu Obasanjo.
0 comments:
Post a Comment