WATU 123 WAFARIKI KWA KUTEKETEA KWA MOTO BAADA YA GARI LA MAFUTA KULIPUKA

 
Watu 123 wamethibitishwa kufa baada ya lori lililokuwa limebeba mafuta kupata ajali na kushika moto kisha kuteketea nchini Pakistan.
Janga hilo limefanyika katika mji wa Ahmedpur Sharqia katika jimbo la Punjap; hayo ni kwa mujibu wa viongozi wa serikali.
Watu wengine kadhaa wameteketea vibaya, pale walipokuwa wakijaribu kuteka mafuta kutoka katika lori hilo la mafuta.
Waliojeruhiwa wanatibiwa hospitali. Wazima moto wamo katika eneo la ajali wakijaribu kukabiliana na moto huo.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zasema kuwa, lori hilo la mafuta lililokuwa likiendeshwa kwa kasi, lilipinduka, kuanguka na kisha kushika moto.
Mashuhuda wanasema kuwa, baadhi ya watu waliofika katika eneo la ajali walikuwa wakivuta sigara, jambo ambalo linakisiwa kuwa chanzo cha moto huo, hiyo ni kwa mjibu wa runinga ya Geo TV ya Pakistan.

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment