Tuesday, June 27, 2017 Lowassa Mikononi mwa Polisi Leo........Ni Kufuatia Wito wa DCI Aliyemtaka Afike Polisi saa Nne

 

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa ametakiwa kuripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) leo  saa nne asubuhi.

Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amepewa wito huo kwa njia ya barau bila kuelezwa sababu za yeye kutakiwa kufanya hivyo.

Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene na Lowassa mwenyewe wote wamethibitisha kupata taarifa za wito huo huku wakisema si chama wala mhusika anayejua sababu za kuitwa.

Aidha, katika mahojiano aliyofanya Lowassa na The Citizen kwa njia ya simu, amesema kuwa anadhani kuitwa kwake kuna uhusiano na kauli aliyoitoa mwishoni wa juma wakati wa futari kuhusu Masheikh wa Uamsho.

Lowassa alimtaka Rais Magufuli kuingilia kati suala hilo ambapo Masheikh kadhaa wanashikiliwa kwa zaidi ya miaka minne sasa bila maendeleo yoyote ya tuhuma zinazowakabili. Masheikh hao ambao walikamatwa Zanzibar wanatuhumiwa kwa ugaidi ambapo Lowassa alitaka Rais aingilie kati ili kesi hiyo iweze kusikilizwa.

“Sina hakika kama hii ndio sababu, lakini nahisi tu. Ila ukweli utafahamika  nitakapokutana na DCI,”  alisema Lowassa kwenye mahojiano hayo ya simu.
 
KAPOLA NEWZ

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment