MAAFISA afya
mkoani Rukwa wameweka
kambi katika mwambao
wa ziwa Tanganyika
sambamba na kugawa
mavazi lasimi ya
yakujikinga na ugonjwa
wa ebora kwa wahudumu wa
afya kwenye zahati
zilizo mpakani mwa nchi
ya Tanzania na
Kongo na huku wenyeviti
wa vijiji wakitakiwa
kutoa taarifa za
haraka pindi kunapotokea
uwepo viashiaria vya
ugonjwa huo.
Hatua hiyo
inakuja baada
ya ugonjwa wa
ebora siku za
hivi karibuni kulipotiwa
kujitokeza nchini kongo
na kuwa hatari
zaidi kwa wananchi
wanaoishi kwenye mwambao
wa ziwa Tanganyika ambalo
liko jilani kabisa na
nchi hiyo.
Akiongea na kituo hiki
wakati wa mafunzo
maalumu kwa viongozi
wa serikali za vijiji na
kata kwenye mwambao
wa ziwa hilo
na kufanyika katika
kijiji cha samazi tarafa
ya Kasanga wilaya
ya kalambo mkoani
hapa, Afsa afya wilayani
humo ,Andondile mwakilima ,
amesema ugonjwa huo
hauna tiba wala chanjo
na kuwataka wananchi
kuacha tabia ya
kutumia maji ya
ziwani na badara yake
kutumia maji yalio chemshwa wakati
wote.
Amesema
kila kiongozi anawajibu
wa kufanya ukaguzi
wa maboti yote
yanayo ingia bila
vibari sambamba na
kuwataka viongozi hao
kuhakikisha maboti yote yanapitia
bandari ya kansanga
kwa ajili ya
ukaguzi.
0 comments:
Post a Comment