Hatimaye
imekuwa! Vinara katika ufisadi wa IPTL/ESCROW Singasinga Seth na
Rugemarila watiwa nguvuni. Huu ni uamuzi mkubwa uliosubiriwa sana. Na
siku zote sikujua kwanini Mhe Rais alikuwa anahofu kuagiza hatua hii.
Sikujua
kwanini, kwasababu wakati wa mnyukano wa hoja hii, Mhe Rais alikuwa
bungeni na alikuwa sehemu ya maazimio ya Bunge kutaka mitambo ya IPTL
itaifishwe na wahusika watiwe nguvuni..
Nakumbuka
nikiwa kwenye kipindi kigumu hata kutishwa kuondolewa kichwa na kuitwa
majina ya wanyama, yeye alikuwa miongoni mwa mawaziri 5, walionidokeza
kwamba ESCROW ni dili nikomae tu mpaka kieleweke!
Nampongeza
Mhe Rais kwa uamuzi huu muhimu uliosubiriwa siku nyingi kuamua hatma ya
ufisadi huu uliomshinda vibaya mtangulizi wake.
Singasinga
huyu alinifungulia kesi kunidai Sh300bn Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka
2014, Agust2015 nikamshinda lakini akaamua kunifungulia upya Mahakama ya
Kisutu akidai Sh100m, zote akidai nimsafishe kuwa yeye na wenzake
hawakuchota zaidi ya 300bn kifisadi.
Kifupi
naomba PCCB na DPP wasituangushe watanzania. Nilipata kuwaza kumwomba
Mwanasheria Mkuu wa Serikali anipe kibali niendeshe kesi na hawa
majabali wa escrow kwani nina ushahidi wakutosha,Sasa nina furaha kwamba
PCCB wameamua kuwaburuza.
Nashauri mambo machache;
1.Mali
zote za wahusika hawa ziwekwe chini ya ulinzi kabla hawajahamisha
umiliki kwani ni muhimu zikakamatwa kusubiri hukumu ya kesi hii ya
Tanzania lakini pia kesi iliyopo Mahakama ya kimataifa ya International
Centre For Settlement of Investment Disputes (ICSID). Ambako Septemba
2016, iliamuliwa tulipe Bank ya SCB-HK kiasi zaidi ya 400bn kwa kuwa
ndio wamiliki halali wa IPTL na wenye share certificate za IPTL..
Mwaka
huu TANESCO imekata rufaa. Najua TANESCO hawajakata rufaa kushinda kesi
bali kuomba wapunguziwe hukumu ifanane na uamuzi wa ICSID wa Feb 2014.
Lakini
kwakuwa Singasinga Seth alisaini hati na Benki Kuu ya Tanzania, kwamba
deni lolote lotakalotokana na migogoro ya IPTL atawajibika yeye na
wenzake wanaomiliki kampuni PAP, ndio maana nasisitiza Mali za watu hawa
zishikiliwe.
2.
Mtambo wa IPTL uwekwe chini ya TANESCO kama ilivoazimiwa na Bunge Nov
2014, tuachane kabisa na kulipa matapeli 7bn kila mwezi ambazo ni malipo
ya capacity charges walizokuwa wanalipwa na serikali hii bila kujali
IPTL imezalisha au haijazalisha umeme.
3.
Mwisho watanzania watambue kwamba huyu Singasinga anaetambulishwa kama
mmiliki wa PAP iliyopora 300bn za escrow kama mmiliki mpya wa IPTL,
mpaka fedha hizo zinaporwa alikuwa anamiliki asilimia50% tu ya kampuni
lakini asilimia 50 zilikuwa zikimilikiwa na kampuni ijulikanayo kama
SIMBA TRUST, inayomilikiwa na watu wasiojulikana. Hawajawahi kutajwa
popote kwenye report zote.
Nilijaribu
kutaka majina yao kwenye Kamati ya Viwanda wakati tukiwahoji BRELA na
hata baadae bungeni Serikali iliendelea kusisitiza kuwa majina hayo ni
SIRI. Hawa ni wahusika muhimu sana wajulikane kwani inawezekana ndio
msingi wa serikali ya awamu ya nne kuibeba IPTL kama mtoto!
Naam,
hongera Mhe Rais kwa hatua hii, nazidi kuomba Mungu kesi hizi zifike
mwisho kwani kwangu leo ni siku muhimu katika kumbukumbu zangu kuliko
Aprili 28, 2015, siku niliyopewa tuzo kwa mapambano dhidi ya ufisadi kwa
rejea ya sakata la ESCROW, kwani tuzo haina maana kama vita haifiki
mwisho.
Mwisho
nishauri asiwepo yeyote wakulindwa kwa Kinga yoyote kwani Katiba na
Sheria vipo kwa ajili ya watanzania na sio watanzania kwajili ya Katiba
na Sheria. Tusipofika huko vita ya UFISADI mkubwa itakuwa ngumu sana
kufika mwisho.
0 comments:
Post a Comment