SERIKALI
katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa
imepiga malfuku kula nyama ya
nguruwe pamoja kusafirisha mifugo kutoka
eneo moja kwenda lingene kutokana na
Homa ya mifugo hiyo malfu kama {ARFICAN SWINE FEVER}
kuibuka na kupelekea zaidi ya
nguruwe 150 kufariki na wengine
wakiwa katika hali mbaya na huku madiwani
wakiomba wataamu wa mifugo kutafuta njia
mbadara ya kudhibiti ugonjwa huo.
Ugonjwa
huo una miezi mitatu tangia
kujitokeza kwake , ambapo ulianzia
katika kitongoji cha masazi na
kusambaa katika kata ya legeza mwendo na
mambwe koswe wilayani hapa na kupelekea
kuwepo malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi
ya mifugo yao kufariki kila
siku na huku ugonjwa huo
ukidaiwa kuto kuwa na tiba wala kinga.
Hali hiyo
imefanya mkuu wa wilaya hiyo Julith
Binyura kuchukua hatua ya kukutana
na wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja
na madiwani kutoka kwenye kata zilizo kumbwa
na adha hiyo na kupiga malfuku
kusafilisha mifugo hiyo kutoka sehemu moja
kwenda nyingine sambamba na kujinja mifugo hiyo
mpaka pale tatizo hilo litakapo kwisha.
Katibu tawala
wa wilaya hiyo Frank Schalwe
amewataka wananchi kuacha
kutumia kitolewo cha mifugo
hiyo ili kuepukana na magonjwa
yasio ya lazima.
Afisa
mifugo wilayani humo wilbrod Kansapa , amesema
wamejipa kukamata nguruwe wote wanao zagaa
mitaani ikiwa ni pamoja kuhakikisha
mizoga yote inafukiwa kutokana na
ugonjwa huo kuto kuwa na tiba wala kinga.
Usikose kushare na kuweka coment,,posted by peter kapola 0764033168
0 comments:
Post a Comment