VIDEO: Yanga walivyolipa kisasi kwa Stand United kwa kuifunga 4-0 leo Feb 3

 
February 3 2017 Yanga waliingia uwanjani kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017 dhidi ya Stand United uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga ambao mchezo wa kwanza wa lifungwa na Stand United goli 1-0 katika uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Leo February 3 2017 waliingia uwanjani kucheza mchezo wao wa marudiano dhidi ya Stand United na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 4-0, magoli yakifungwa na Donald Ngoma dakika ya 17, Simon Msuva dakika ya 26, Obrey Chirwa dakika ya 45 na Nadir Haroub Canavaro dakika ya 68.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuendelea kusalia kilele mwa msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 kwa kufikisha jumla ya point 49, hivyo kwa sasa Yanga wanaongoza Ligi kwa kuizidi Simba point nne na wameizidi Simba mchezo mmoja ambapo Simba atacheza kesho dhidi Majimaji FC mjini Songea.

 
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4


VIDEO: Yanga walivyolipa kisasi kwa Stand United kwa kuifunga 4-0 leo Feb 3


Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment