Ghana ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa na mashabiki wengi wa soka kuwa wanaweza kufanya vizuri zaidi katika mchezo huo wa nusu fainali na kuingia fainali, walijikuta wakiruhusu kufungwa dakika ya 72 ya mchezo na dakika za nyongeza wakiwa wanahangaika kusawazisha walifungwa goli la pili kwa shambulizi la kushitukiza.
Magoli ya Cameroon yalifungwa na Michael Ngadeu dakika ya 72 kabla ya Christian Bassogog kuzima ndoto za Ghana kucheza fainali dakika za nyongeza, ushindi huo unaifanya Cameroon kutinga fainali ya AFCON 2017 na watacheza na fainali dhidi ya Misri, fainali ambayo itakuwa inajirudia ya mwaka 2008 ambapo Misri alimfunga Cameroon na kutwaa taji lake la sita.
VIDEO: Fainali ya AFCON 2017 ni Misri vs Cameroon, bye bye Ghana
0 comments:
Post a Comment