Moja kati ya stori kubwa iliyokuwa ikijadiliwa kwa wapenda soka bongo leo ni kuhusiana na habari za nyasi bandia za timu ya Simba kuandikwa kuwa zitapigwa mnada na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutokana na kushindwa kuzilipia kodi bandarini, Simba waliomba msamaha wa kodi lakini imeshindikana.
Lakini kuna taarifa pia zilizotolewa baadae kuwa mtanzania
Mbwana Samatta aliyewahi kucheza
Simba ambaye kwa sasa anaichezea
KRC Genk ya
Ubelgiji amezilipia kodi hizo, ukweli kutoka katika ukurasa rasmi wa msemaji wa Simba
Haji Manara na
TRA ni kuwa
Samatta hajalipia kodi ya nyasi hizo.
Ukweli wa taarifa rasmi ni kuwa
Simba wameongezewa
muda wa siku 14 wazilipie kodi nyasi zao hizo bandia ambazo wanampango
wa kuziweka katika uwanja wao wa mazoezi wa
Bunju, katika siku 14 walizopewa
Simba tayari zimebakia siku tatu pekee.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment