eshi la Polisi nchini Tanzania
linamshikilia mwanamuziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki, alimaarufu
kama Ney wa Mitego kuhusiana na wimbo wake alioutoa hivi karibuni, mwa
mujibu wa vyombo vya habari nchini humo
Gazeti la Mwananchi linaripoti kwamba Ney wa Mitego, alikamatwa mnamo majira ya saa nane usiku wa kuamkia siku Jumapili katika mkoa wa Morogoro, kilomita 200 kutoka jijini Dar es Salaam, kwa kosa la kutoa wimbo unaoikashifu serikali
Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita huku sehemu ya maudhui ya wimbo huo ukigusia tuhuma za kughushi vyeti ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari nchini Tanzania
- Wema Sepetu na wasanii wenzake mbaroni kwa mihadarati Tanzania
- Mshukiwa mkuu wa mihadarati akamatwa Tanzania
- Washukiwa 13 mahakamani kwa tuhuma za mihadarati Tanzania
Matei alisema Ney wa Mitego angepelekwa jijini Dar es Salaam ambako ndipo shauri lake lilipo na kuhojiwa zaidi na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa juu ya kazi zake za kisanaa
0 comments:
Post a Comment