Baadhi
ya wasanii wa kundi la Mama Ongea na Mwanao, waliokuwa katika kampeni
za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 za mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mama Samia Suluhu, wamekanusha madai ya kutolipwa wala kukidai
chama hicho madeni yoyote wakati na baada ya kampeni hizo kumalizika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam leo, Makamu
Mwenyekiti wa muda wa kundi hilo, Yobnesh Yusuph maarufu Batuli,
alisema madai hayo si kweli kwani wasanii wote walilipwa na mikataba
wanayo.
“Nikiwa kama Makamu Mwenyekiti wa ‘group’ hili la Mama Ongea na Mwanao
kwa muda, ni kweli kuna uvumi ulienea katika mitandao kwamba wasanii
tulioshiriki kampeni na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu hatujalipwa,
si kweli nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli.
“Ingawa kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani, wapo wanaoshawishiwa
kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais na kuichafua CCM, mimi
nakataa, wasanii wote tulilipwa na mikataba ipo.
"Haiwezekani wewe staa mkubwa unakaa mbele ya vyombo vya habari unaongea
uongo kwamba wasanii hatujalipwa wakati wewe ndiyo ulikuwa unawalipa
hicho kitu hakiwezekani,” alisema Batuli aliyekuwa ameongozana na baadhi
ya wasanii wa kundi hilo.
Hivi karibuni msanii nyota wa filamu na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu
ambaye alitoka CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), alisema wasanii hao wanadai malipo yao ambapo hakutaja kiasi
wanachodai na kwamba wamekuwa wakizungushwa pindi wanapoulizia madeni
hayo.
0 comments:
Post a Comment