NAPE AMSHUKURU RAIS KWA KUMUAMINI KWA MWAKA MMOJA, APONGEZA PIA UTEUZI WA MWAKYEMBE

na2 
 
Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewataka Watanzania kukubaliana na suala la  kusitishwa kwake uteuzi wa cheo hicho.
Rais John Magufuli amemteua Dk Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi hiyo ya Nape.
Akizungumza na waandishi nje ya Hoteli ya Protea, leo. Nape amesema wanatakiwa kukubaliana na hali halisi.
“Mkubali Tanzania ni kubwa kuliko Nape na hampaswi kuanzisha matatizo. Tanzania ni nchi yetu sisi na tujue Nape hawezi kuwa mkubwa kuliko Tanzania.
“Nawashauri kuwa watulivu, namshukuru Rais Magufuli kwa kunipa nafasi ya kufanya naye kazi kwa mwaka mzima.
“Nilifanya kazi yangu kwa akili na nguvu zangu zote. Nawashukuru wasanii, waandishi, wanamichezo kwa ushirikiano wenu. Nilipenda kuendelea kufanya kazi nanyi lakini muda wa aliyeniteua umefika, nitawakumbuka sana, ninawapenda sana,” alisema Nape.
Wakati anataka kuondoka katika eneo hilo, gari lake lilizuiwa na RPC wa Kinondoni, Suzan Kaganda hali iliyosababisha taharuki hadi Nape aliwapowaomba waandishi kuondoka eneo hilo ili naye aondoke.

na3
 
na1 
 
Baadhi ya maaskari wakiwa wameimarisha ulinzi katika eneo hilo.
 
na4 
 
Gari la Kamanda wa polisi mkoa wa Kindondoni likiwa katika eneo la tukio.
 
  
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment