Kiongozi mkuu wa Upinzani nchini
Urusi Alexei Navanly, amekamatwa wakati wa maandamano ya kupinga ufisadi
aliyoandaa kwenye mji mkuu Moscow.
Navalny ni maarufu kwa kampeni zake za kupinga ufisadi ambazo huwalenga maafisa wa vieo vya juu walio karibu na serikali ya Urusi.,
Anazuiwa kuwania urais kumpinga rais Vladimir Putin mwaka ujao, baada ya kupatikana na hatia kati ya kesi anayoitaja kuwa ilichochewa kwa misingi ya siasa.
Waandamanaji kadha walikamatwa, pale polisi walipojaribu kuvunja maandamano katika mji wa Vladivostok, kando ya Bahari ya Pacific.
Waandamanaji huko Chelyabinsk, walitaka Waziri Mkuu, Dmitry Medvedev ajiu-zulu kuhusu tuhuma za ufisadi.
0 comments:
Post a Comment