AyoTV VIDEO: Waziri Muhongo alivyozindua mradi wa umeme Kagera

 

Waziri wa Nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo leo March 30, 2017 amezindua ujenzi wa mradi wa umeme wa maporomoko ya mto Rusumo ambao unatarajia kuwa na megawati 80 zitakazosaidia kuongeza nguvu ya nishati ya umeme kwa nchi tatu,Tanzania,Rwanda na Burundi.
Mradi huo utagharimu U$D million 340 kutoka Benki ya dunia, ambapo benki ya maendeleo ya Afrika itatoa U$D million 121,na baada ya mradi kukamilika kila nchi inatarajia kupata megawati 26.6.
Pia Prof.Muhongo amesema kuwa mradi huo unatarajia kukamilika February 2020 huku akitoa ufafanuzi wa fidia kwa wale watakaopisha mradi huo unaojengwa katika eneo la Rusumo lililopo wilaya ya Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda.




Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment