Serikali
imepiga marufuku tabia ya baadhi ya waalimu kutoa adhabu kali na za
kikatili kwa wanafunzi na badala yake waalimu wameelekezwa kutoa adhabu
kulingana na taratibu na sheria zilizowekwa.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. George
Simbachawene kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Msaidizi
kutoka Ofisi ya Rais katika uzinduzi wa ripoti ya elimu ya msingi nchini
amesema, kumekuwa na tabia ya baadhi ya waalimu kutoa adhabu kinyume
cha taratibu.
Naye
Mratibu wa Mtandao wa Elimu nchini ambao ni wasimamizi wa utafiti huo
Bi. Cathrene Sekwao na mtafiti Bw. Jacob Kateri amesema wameamua kufanya
utafiti huo ili kuweza kujua hali ya elimu ikoje ili serikali iweze
kuona nini kifanyike kuboresha sekta ya elimu ambapo pia wameitaka
serikali kupitia mapendekezo yao.
KAPOLA NEWZ
0 comments:
Post a Comment