Mkazi
wa kijiji cha Kate, wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa, amejikata uume wake
kwa kisu kwa hasira baada ya kuota kuwa anafanya mapenzi na mke wake
aliyefariki mwaka mmoja uliopita.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 58 alijikata uume wake juzi majira ya
saa 4:00 asubuhi akiwa amejifungia chumbani kwake peke yake.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Richard Mselema, akizungumzia tukio hilo
alisema kuwa, mtu huyo alikuwa akitafuta binti wa kumuoa na kuishi nae
kwa muda mrefu baada ya mke wake kufariki, lakini wanawake wamekuwa
wakimkataa kwa kuwa umri wake ni mkubwa.
Baada ya kufanya tukio hilo akiwa peke yake na kupata maumivu makali,
mwanaume huyo alipiga yowe na watu walipofika na kumkuta anavuja damu
nyingi sehemu ya uume wake huku kisu kikiwa kimetupwa pembeni, waliamua
kumbeba na kumkimbiza katika Zahanati ya Kate Mission.
Kwa mujibu wa daktari wa zamu, Paul Katindi, aliyempatia matibabu katika
majeraha aliyoyapata, alisema kuwa hali yake itakuwa nzuri na anaweza
kuendelea na mchakato wake wa kumtafuta mwanamke wa kuoa.
“Niliamua kujikata kutokana na kuwa na uume lakini siutumii kwa kuwa
sina mke wala mpenzi. Hivyo sikuona umuhimu wala faida ya kuwa nao.”
Alisema majeruhi huyo alipoizungumza na mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Nkasi, Zeno Mwanakulya, ambae pia ni jirani yake, alipokwenda
kumtembelea na kumpa pole.
0 comments:
Post a Comment