SERIKALI katika
wilaya ya Kalambo
mkoani Rukwa imefanikiwa
kutenga maeneo yenye ukubwa
wa hekari 15 kwa
ajili ya ujenzi
wa viwanda sambamba na kutenga hekari 280 kwa ajili
ya ujenzi wa
makazi , biashara, na ofisi
mbalimbali za serikali.
Akiongea na
kituo hiki kaimu mkurugenzi wa
halmashauri hiyo frenki
Fuko wakati wa kikao
maalumu cha utendaji ,amesema kwa
kutambua sheria ya mipango miji , hivyo serikali
kupitia idara ya ardhi imefanikiwa
kupima viwanja 280
ambavyo vitatumika kwa
matumizi ya makazi , biashara , na ujenzi
wa ofis mbalimbali za serikali
kwa lengo la kudhibiti
ujenzi holela wa mkazi.
kaimu afisa aridhi
wa wilaya hiyo Richard Ngaitta amesema licha
ya hilo serikali
kupitia idara hiyo
pia imefanikiwa
kutenga hekali 15
ndani ya mamlaka
ya mji wa
Matai kwa ajili
ya ujenzi wa viwanda.
Mkuu wa
wilaya hiyo Julith
Binyura amesema
licha ya maeneo
hayo kutengwa , pia serikali
wilayani humo inaendelea
kutenga maeneo mengine
na kuwataka wananchi
na mashirika binafus
kufika wilayani humo
ili kuwekeza kwenye viwanda.
0 comments:
Post a Comment