Semina ya wafanyabiashara wamafuta leo march 31 mkoani Rukwa

http://1.bp.blogspot.com/-8B7BlABxUxs/VK4lDvMnzQI/AAAAAAADLbI/wmOx6l1Hs7U/s640/IMG_2394.JPG 

Mkurugenzi wa Eura Godwini Samweli mkoani Rukwa,picha na Peter kapola

SUMBAWANGA MARCH 31

Wafanyabiashara wa mafuta nchini hii leo wamefanya Semina iliyo husisha changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo ikiwa ni pamoja na kuziangalia sheria na kanuni katika udhibiti wa secta ya petroli nchini.

Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wafanyabiashara ambao walihudhulia semina hiyo iliyo fanyika wilayani sumbawanga katika ukumbi wa Halmashauri mkoani Rukwa wameeleza changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na suala la baadhi ya wafanyabiashara kuuza mafuta kwa bei za juu.

Hata hivyo kwa upande mwingine wafanya biashara hao wameuomba uongozi wa EURA kuweza kuweza kuwachukulia hatua za kisheria kwa wale wanao uza mafuta ya rejareja kwenye magali sambamba na wanao safilisha nje ya nchi bila kufuata taratibu na sheria za kusafilisha mafuta.

Nae mkurugenzi wa EURA GODWINI SAMWELI amesema kwa wale wafanyabiashara wanao uza mafuta kwa bei za juu waweze kuacha mala moja na kuwaomba wateja kutoa taarifa pale watakapoona mafuta yanauzwa kwa bei ambayo sio elekezi.

Pia amewataka wafanyabiashara wote wanao uza mafuta ya rejareja kuweza kuacha kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanahatalisha usalama wa wananchi na taifa zima kwa ujumra.
 
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment