YANGA YAJIPANGA KUUA NDEGE MAWILI KWA WAKATI MMOJA


Kikosi-CHa-Yanga-2016-2017-Bongosoka 

Na.Alex Mathias,Dar es salaam

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga wanaendelea na mazoezi yao ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu na kombe la FA pamoja na Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF.

Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi hayo baada ya kuondoshwa katika Michuano ya kombe la klabu Bingwa Afrika na wamekiwa wakifanya kazi iyo katika uwanja wa Polisi Kurasini,Kilwa jijini Dar es salaam.

Yanga inaendelea kujifua kwa kuwa pamoja na Ligi Kuu Bara, wanatakiwa kuendelea kuwa fiti kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho bila ya kocha wao Mkuu George Lwandamina pamoja na baadi ya wachezaji ambao wameitwa katika timu za Taifa huku Washambuliaji wao hatari wawili bado wana majeruhi.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema wachezaji wako katika hali nzuri isipokuwa Amis Tambwe na Donaldo Ngoma bado hawajaanza mazoezi na katika mechi dhidi ya Azam FC hawatakuwepo.

“Mazoezi ni kawaida ya kuendelea kujiweka vizuri lakini wachezaji wako vizuri japokuwa kikosi kamili hakijakamilika kutokana na sababu mbalimbali,” alisema.

Yanga imekuwa na msimu bora kabisa katika msimu uliopita lakini tofauti na msimu huu, inaonekana mambo hayajakaa vizuri sana hii ni baada ya mwenyekiti wao Yusuf Manji kutajwa kwenye sakata la madawa ya kulevya pamoja na accounti zake kufungiwa na Serikali na mpaka sasa yupo chini ya ulinzi huku akiwa katika Hispatili ya Aghakan.

Yanga wanatarajia kucheza na Azam FC April Mosi mchezo wa Ligi kuu na baada ya hapo watashuka dimbani Aprili 7,8 au 9 kucheza na MC Alger ya Algeria kwenye Michuano ya kombe la shirikisho kuwania nafasi ya kuingia hatua ya makundi


Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment