Polisi 40 wauawa kwa kukatakatwa Kasai, DR Congo

Tshimbulu, Kasai , 20 Machi 2017 

Wanamgambo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamewashambulia na kuwaua kwa kuwakatakata wanajeshi takriban 40 baada ya kuwavizia katika mkoa wa Kasai, katikati mwa nchi hiyo, maafisa wa serikali wamesema.

Wapiganaji hao kutoka kundi la Kamwina Nsapu walishambulia polisi waliokuwa kwenye msafara.
Maafisa sita wa pilisi waliowasiliana na Tshiluba waliachiliwa huru, rais wa bunge la jimbo la Kasai Francois Kalamba amesema.

Machafuko jimbo la Kasai yalianza Agosti mwaka jana, pale maafisa wa polisi walipomuua kiongozi wa Kamwina Nsapu.
Shambulio la Ijumaa lililenga msafara wa polisi waliokuiwa wakisafiri kati ya Tshikapa na Kananga.
Gavana wa jimbo hilo Alexis Nkande Myopompa amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu mauaji hayo.

Umoja wa Mataifa unasema watu 400 wameuawa na wengine 200,000 kuachwa bila makao eneo la Kasai tangu Jean-Pierre Pandi, kiongozi wa Kamwina Nsapu alipouawa.

Mauaji yake yalitekelezwa miezi miwili baada ya Kamwina Nsapu mwezi Juni 2016 kuanzisha juhudi za kutaka atambuliwe kama mkuu wa eneo hilo na kutaka maafisa wa serikali ya taifa kuondoka jimbo hilo.

map
Umoja wa Mataifa unasema umepata makaburi 10 ya pamoja ambapo waliouawa katika machafuko hayo walizikwa.

Kadhalika, kuna maeneo mengine saba ambapo inadhaniwa kuna makaburi yaliyozikwa watu wengi kwa pamoja.

Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa, Mmarekani na raia wa Sweden, walitekwa nyara eneo hilo wiki mbili zilizopita pamoja na raia wanne wa DR Congo waliokuwa wakifanya kazi nao.
Kufikia sasa bado hawajulikani walipo.

Mwanajeshi wa Congo akiwa Goma, Dr Congo, Novemba 12, 2008
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wa usalama DR Congo wamekuwa wakikabiliana na waasi maeneo mbalimbali nchini humo
DR Congo imekabiliwa na hali ya wasiwasi kisiasa huku Rais Joseph Kabila akiendelea kukaa madarakani kwa muda zaidi kuliko alivyoruhusiwa kikatiba.
Muhula wake ulimalizika Desemba mwaka jana.
Uchaguzi umepangiwa kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu lakini tarehe kamili haijaafikiwa.

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment