Wakulima
wanahitaji kuwezeshwa kuendesha kilimo cha kisasa kama hiki ili waweze
kupata mazao ya kutosha na kuboresha maisha yao ,mpango wa TBL Group
kushirikiana na wakulima utasaidia kuleta mabadiliko
Wakulima
wanahitaji kuwezeshwa kuendesha kilimo cha kisasa kama hiki ili waweze
kupata mazao ya kutosha na kuboresha maisha yao ,mpango wa TBL Group
kushirikiana na wakulima utasaidia kuleta mabadiliko hapa anaonekana mmoja wa wakulima akina mama akivuna mtama.
Mikakati madhubuti inahitajika kuwapatia wakulima nyenzo za kisasa badala ya kutumia jembe la mkono
Wakulima wanaoshirikiana na TBL mkoani Arusha wakipata maelezo ya kitaalamu katika mashamba yao ya Shahiri
Wakulima wanaoshirikiana na TBL mkoani Arusha wakipata maelezo ya kitaalamu katika mashamba yao ya Shahiri
………………………………………………………………………………….
*Mkakati huu kunufaisha maelfu ya wananchi kwa kuboresha maisha yao na kukuza wigo wa ajira
Kampuni ya TBL Group imeeleza kuwa pamoja na kuweka kipaumbele utekelezaji mkakati wa serikali wa ukuzaji
sekta ya viwanda nchini pia itaendelea kushirikiana na wakulima
wanaozalisha malighafi kwa ajili ya viwanda vyake ili kuhakikisha sekta
ya kilimo inakua na kutoa mchango katika pato la taifa ikiwemo kuboresha maisha ya wakulima nchini.
Hadi kufikia sasa utekelezaji wa mpango wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wakulima wadogo wadogo ambao umeanza kutekelezwa na
kampuni hiyo kwa wakulima wa zao la Shahiri kanda ya Kaskazini mwa
Tanzania na wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma umesaidia kuongeza ajira
ikiwemo kuboresha maisha ya wakulima.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ambaye pia ni Mkuu wa Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin, amesema katika mahojiano maalumu, kuwa
mpango wa kilimo shirikishi unaotekelezwa katika mikoa ya Arusha na
Kilimanjaro mbali na kuinua hali za maisha ya wakulima pia unanufaisha
wananchi zaidi ya 3,000 wanaojipatia ajira katika utekelezaji wake na
kwa upande wa zao la Zabibu zaidi ya wakulima 700 mkoani Dodoma wamenufaika.
“Moja
ya sera ya kampuni yetu ya “Dunia Maridhawa”-(Better World) inalenga
kuwezesha wakulima katika maeneo tunayofanyia biashara zetu na kuwezesha
jamii kuwa na maendeleo endelevu katika shughuli za maisha yao ya kila siku”.Alisema.
Aliyataja
makundi ya wawaonufaika na mpango huu kuwa ni vibarua wanaofanya kazi
mashambani kwa kupuliza dawa mashambani,madereva wa matrekta wanaolima
mashamba na kuvuna,vibarua wa kupakia mazao na kuyashusha,wasafirishaji
na watengenezaji na magunia ya kupakia mazao.
Alisema Mbali na wanaonufaika katika hatua mbalimbali za utekelezaji wakulima wa zao la Shahiri katika mikoa ya Kaskazini ya Arusha na Kilimanjaro tayari wameanza
kuonja matunda ya ushirikiano huu kwa kuwa wanawezeshwa kuendesha
kilimo cha kisasa,kupatiwa pembejeo,mbegu na wataalamu wa kutoa ushauri
na wanakuwa na soko la uhakika kwa ajili ya kuuza mazao yao,hali ambayo
imebadilisha hali zao za maisha kuwa bora.
“Mpango
wa kampuni wa kushirikiana na wakulima haulengi kunufaisha wakulima wa
Shahiri na Zabibu pekee bali pia wa mazao mengine kama mtama na mihogo
na katika siku za usoni wakulima wa zao la mahindi watawezeshwa pia na
wananchi wengi watajipatia riziki kutokana na kufanya kazi za utekelezaji wake”.Alisema
Mpango huu wa kampuni kutegemea kupata malighafi kutoka hapa
nchini umeungwa mkono na serikali za nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania
kwa kuwa unalenga kuinua hali za maisha za wananchi hasa wakulima ambao
wana hali duni kutokana na changamoto nyingi zilizopo katika sekta ya
kilimo.
Huu
ni mfano wa uwekezaji wenye faida kwa watanzania kwa kuwa unaeleta
mabadiliko kwenye jamii na kubadilisha maisha ya wananchi wengi kuwa
bora.
0 comments:
Post a Comment