Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndg. Andrew W. Massawe akimpokea
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba(Mb) mara baada ya
kuwasili katika ofisi za NIDA makao makuu.
wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge wakiongozwa na
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Adad Rajab (Mb) wakiwasili katika makao
makuu ya ofisi za NIDA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba (MB)
akisalimiana na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge Mh.
Adad Rajab (Mb) wakati wa ziara ya kamati hiyo katika ofisi za NIDA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba
akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na
Usalama walipowasili NIDA kutembelea na kukagua maendelea ya mradi wa
Vitambulisho vya Taifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na
Usalama Mh. Adad Rajab (Mb), akiongea jambo wakati wa kikao na
Menejimenti ya NIDA baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji toka kwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw. Andrew W. Massawe. Kulia ni Makamu
mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Kanali Mstaafu Ramadhani Issa
Abdallah(Mb).
Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo
Nje, Ulinzi na Usalama leo imefanya ziara ya kukagua mradi wa
Vitambulisho vya Taifa; ambapo mbali na kupokea taarifa ya utekelezaji
pia walitembelea na kukagua kituo kikuu cha Kuhifadhi, kuchakata na
kuzalisha Vitambulisho vya Taifa -Data Centre.
Akizungumza wakati wa
kukaribisha Kamati hiyo; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu
Lameck Nchemba (Mb) amesema mpaka sasa NIDA imefanikiwa kutekeleza
majukumu yake kwa kiwango kikubwa pamoja na changamoto kubwa ya fedha
iliyopo.
Akizungumza kwa niaba ya
Kamati hiyo; Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Adad Rajab (Mb) amepongeza
jitihada kubwa zinazofanywa na NIDA na kwamba Kamati imeridhishwa na
kazi kubwa na nzuri inayofanywa na NIDA na kwamba Kamati yake itaendelea
kuishauri Serikali kuongeza bajeti ya fedha kwa NIDA ili kuwezesha
kukamilisha zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa, kwani manufaa ya
kuwa na mradi huu kwa Taifa ni makubwa katika Nyanja zote.
Wakitoa maoni yao wajumbe wa
Kamati hiyo wameitaka Wizara kuiwezesha NIDA na kuharakisha matumizi ya
Vitambulisho vya Taifa kielektroniki kwani tayari idadi kubwa ya
wananchi wameshatambuliwa na taarifa zao kuingizwa kwenye mfumo.
“Kutokana na manufaa makubwa
ya mradi huu kwa Taifa, Serikali ihakikishe inatumia kila mbinu
kuhakikisha matumizi yaliyokusudiwa ya kuwa na Vitambulisho vya Taifa”
Akisoma taarifa yake kwa
Kamati hiyo; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Andrew W. Massawe
ameieleza Kamati hiyo mpaka sasa NIDA imekamilisha Usajili wa Watumishi
wa Umma nchi nzima ambapo watumishi 500,605 wamesajiliwa, NIDA imeanza
kuwasajili wageni wanaoishi kihalali nchini, kufungua ofisi katika
Wilaya zote nchini pamoja na kuanza zoezi la kuwasajiliwa wananchi
katika mikoa mbalimbali nchini akiitaja baadhi; Lindi, Iringa, Geita,
Singida, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Manyara n.k.
0 comments:
Post a Comment