Mtu mmoja ameuawa na wengine 14 kujeruhiwa kufuatia ufyatuaji wa risasi kwenye klabu ya usiku huko Cincinati jimbo la Ohio.
Watu kadha walipata majeraha mabaya.
"Tuko kati kati ya hali mbaya alisema mkuu wa polisi" Paul Neudigate.
Kapteni wa polisi Kimberly Williams alisema kuwa polisi hawana taraifa kuhusu washambuliaji hao.
- Aliyewaua watu 5 Marekani akamatwa
- Aliyewaua watu 5 Marekani afunguliwa mashtaka
- Maadhimisho ya mauaji ya mweusi Marekani
Ufyatuaji huo ulitokea saa 05:00 GMT wakati mamia ya wtu walikuwa eneo hilo.
Kisa hicho kinatokea chini ya mwaka baada ya Omar Mateen, kufyatua risasi kwenye klabu ya wapenzi wa jinsia moja mjini Orlando huko Florida.
Mateen aliwaua watu 49 katika kisa ya kibaya zaidi cha ufyatuaji risasi katika historia ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment