Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kiwanda
cha Kuchakata Gesi Asilia Madimba wa Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC), mkoani Mtwara, Mhandisi Sultan Pwaga, wakati Naibu
Waziri huyo alipofanya ziara kiwandani hapo kuangalia jinsi gesi
inavyozalishwa. Hata hivyo, Masauni alitoa ahadi, Jeshi lake litafanya
taratibu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda
(katikati) pamoja na TPDC kufanikisha uwepo wa Kituo cha Polisi kama
walivyoomba uongozi wa Kiwanda hicho kwa ajili ya kuimarisha ulinzi
kiwandani hapo pamoja na wananchi waishio jirani na kiwanda hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) akizungumza na Wananchi wa Kijiji
cha Kilambo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Masauni
aliwataka wananchi hao kudumisha amani mpakani hapo pamoja na kufuata
sheria za uhamiaji za nchini pamoja na za Uhamiaji Msumbiji endapo
watahitaji kuvuka mpaka huo. Masauni baada ya kukagua mpaka huo
aliwataka maafisa wakekuimairisha ulinzi zaidi mpakani hapo. Wapili
kulia ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni(katikati) akiiangalia moja ya nyumba za askari wa Jeshi la
Magereza ambazo zinahitaji marekebisho katika Gereza Lilungu mkoani
Mtwara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya
Mtwara, Evod Mmanda. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi hilo mkoani humo, Ismail
Mlawa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto)
akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuhitimisha ziara yake kukagua
mpaka wa Tanzania na Msumbiji uliopo katika Kijiji cha Kilambo, mkoani
Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda. Wapili kulia
ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama, na Mkuu wa Jeshi la Polisi
mkoa huo, Neema Mwanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwapa maelekezo maafisa wake
wakati alipokuwa Mto Ruvuma, Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani mwa
Tanzania na Msumbiji, mkoani Mtwara.Wapili kushoto ni Afisa Uhamiaji
mkoa huo, Rose Mhagama, na anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa
huo, Neema Mwanga.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Jeshi
la Magereza Mkoa wa Mtwara, Ismail Mlawa kwa ajili ya kwenda kukagua
nyumba za askari Magereza wa Gereza Lilungumkoani humo ambazo zinahitaji
marekebisho kutokana na kuharibika. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment